Sunday, February 21, 2016

Azimio La Kwaresima Katika Mwaka Wa Jubilei Ya Huruma ya Mungu

Ukitaka kufunga Kwaresima ya Mwaka huu wa Huruma ya Mungu vizuri kama Baba Mtakatifu anavyotuasa katika tafakari zake wakati huu na kama unataka kubadilisha kweli sura ya maisha yako na Ukristo wako, timiza yafuatayo anayotushauri Baba Mtakatifu Fransisko:
 • funga maneno yanayoumiza wengine na tamka maneno yanayojenga na kufariji 
 • funga hisia zako za huzuni na ujaze roho yako hisia za shukrani 
 • funga hasira yako na ujae subira na uvumilivu 
 • funga hisia zako za kukata tamaa na ujae matumaini 
 • funga msongo wa mawazo yako na umtumainie Mungu 
 • funga malalamiko yako na tafakari kwa shukrani kila ulicho nacho 
 • funga changamoto zinazokuletea presha na ukuze maisha yako ya sala 
 • funga hisia za uchungu na za kuonewa na ujaze moyo wako hisia za furaha 
 • funga tabia ya uchoyo na ubinafsi na ujenge tabia ya wema na huruma kwa wengine 
 • funga ubishi wako na ugomvi na upatane na wenzio 
 • funga maneno na unyamaze ili uweze kuwa msikilizaji makini

No comments:

Post a Comment