Monday, January 2, 2012

Sub Tuum Praesidium!

These are the words I spoke while kneeling yesterday in front of the main altar of Divine Mercy Shrine in Kiabakari. When I was getting ready for the New Year Masses in my mission, on the first day of the New Year 2012, on the Solemnity of Holy Mary, Mother of God, I felt a very strong urge to consecrate my mission anew to Our Lady...


Following this spiritual desire, right after the Gospel in each Holy Mass, I explained the purpose of this spiritual exercise to the liturgical assembly and knelt down to say the consecration prayer which I prepared years ago, during the celebrations of the Great Jubilee Year 2000, based on the consecration prayer written by Blessed John Paul II.

When I came back home after the Thanksgiving Mass on New Year's Eve, it struck me particularly hard that what is coming up in 2012, what we planned, what we wish to achieve, what needs to be done and especially things and challenges which may come up suddenly, thrown at us, constitute a huge mountain to climb for feeble human beings like me and my community. The sudden thought of consecration of the parish and the New Year 2012 to maternal care of Our Lady came as a instant relief to my apprehension and tension.

Having read aloud the words of the prayer in front of the altar, I felt such a wave of calmness, serenity and inner joy, that I knew that Our Lady has had accepted our act of consecration to Her. That is why I feel so much more positive and reassured that with Her help and guidance we will be able to fulfill the Lord's Will the best we can.

These are the words of the act of consecration of Kiabakari parish to Our Lady. Feel free to copy the text and use it for your own spiritual benefit:




“Tunakimbilia ulinzi wako, Mzazi Mtakatifu wa Mungu!”
1. Kwa maneno ya antifona hii inayosaliwa na Kanisa la Kristo tangu karne nyingi, twasimama leo mbele yako, Mama, tunapoingia katika Mwaka Mpya wa 2012.
Twasimama mbele yako tukiungana sote kama familia moja ya Watoto wa Mungu – Mapadre, Watawa, Makatekista, Viongozi walei na waumini wote – tukiwa mwili mmoja na roho moja katika Kristo chini ya Mchungaji mmoja wa Jimbo letu la Musoma, Baba Askofu, anayemwakilisha Kristo mwenyewe kwetu.
Katika roho ya umoja huo twatamka maneno ya sala hii ya kuiweka wakfu Parokia yetu kwako, Mama; sala, ambayo kwa njia yake twataka kwa mara nyingine tena kueleza matumaini na mashaka ya Parokia yetu katika ulimwengu huu geugeu wa kisasa.
Waasisi wa Parokia yetu, wakiongozwa na Roho wa Bwana, waliweka Parokia yetu ya Kiabakari chini ya Usimamizi wako, Mama, wakikukabidhi Parokia hii pamoja na watu wake wote na hatima ya safari ya kiroho ya kila mmoja wao katika dunia hii.
Sisi, waandamizi wa waasisi wetu, twaja tena mbele yako, Mama, kama familia moja ya Watoto wa Mungu na Watoto wako pia chini ya Ulinzi na Malezi yako, Mama, turudie tendo hilo la waasisi wetu la kuikabidhi na kuiweka wakfu Parokia yetu kwako, Mama wa Yesu!
Mama-Kanisa katika Mtaguso wa Pili wa Vatikano alijikumbushia wajibu wa utume wake hapa duniani, kama Yesu mwenyewe alivyomwagiza: “Enendeni ulimwenguni mwote mkiwafundisha mataifa yote…nami nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahari” (Mt 28,19-20).
Kwa sababu hiyo, ee Mama wa wanadamu na wa mataifa, Wewe unayeelewa mateso yao yote pamoja na matumaini yao yote; Wewe unayefahamu mapambano ya wanaparokia wote dhidi ya utawala wa giza katika maisha yao, tunakuomba ukipokee kilio chetu kwako katika Roho Mtakatifu! Utupokee sisi kwa upendo wako wa Mama na Mjakazi wa Bwana. Uipokee tena na upya Parokia yetu na watu wake wote! Uipokee hatima ya safari ya maisha ya kila mmoja wetu! Umwombee kila mmoja wetu neema ya kufika salama nyumbani kwa Baba wa Mbinguni!
Tunakukabidhi na kuwaweka wakfu kwako Mapadre wetu, Watawa, Makatekista, Viongozi Walei, wagonjwa, wahitaji wa kila namna, watoto, vijana, wanandoa, wanafamilia na wazee. Kwa namna ya pekee tunawaweka wakfu kwako wadhambi, walioasi dini, walioanguka katika imani yao, maskini, watoto wa mitaani, familia zilizovunjika, waathirika wa UKIMWI, wasioweza kupata ajira, wanaoteseka kisaikolojia, kiroho na kimwili.
„Tunakimbilia ulinzi wako, Mzazi Mtakatifu wa Mungu! Usituache tukikuomba katika shida zetu!”
2. Ututazame, ee Mama wa Kristo! Tupo hapa mbele yako! Twataka pamoja na Kanisa zima la Mungu kujiunga leo na sadaka ya Mwanao altareni katika Misa hii Takatifu ambaye kwa ajili ya upeo wa upendo wake kwetu alijitoa sadaka kwa Baba yake wa mbinguni: „Kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli” (Yn 17,19). Twataka kuungana na Mkombozi wetu katika sala yetu hii ya leo ya kujiweka wakfu kwako, Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Mama wa Mkombozi! Tunajiweka wakfu kwako, Mama, kwa ajili ya ukombozi wa wanaparokia wote walioko Toharani, walioko safarini kuelekea Mji wa Mwanga wa Mbinguni na kwa ajili ya sifa ya wanaparokia wenzetu washindi walioko mbinguni.
Nguvu ya kujiweka wakfu kwetu idumu milele hata mwisho wa nyakati. Nguvu yake imshinde kabisa Yule Mwovu na utawala wake wa giza katika mioyo ya watu!
Lo, jinsi gani tunajisikia tunahitaji kujiweka wakfu kwako, ee Mama yetu Mwema! Ni hitaji iliyoje mioyoni mwetu! Kazi ya Ukombozi wa Mwanao iendelee kupitia kwa nia yetu ya kujiweka wakfu kwako, Mama wa Yesu Kristo!
Uheshimiwe, ubarikiwe kwa namna ya pekee katika kipindi hiki kitakatifu, ee Mama wa Mungu! Wewe, uliye mfano bora wa kutimiza mapenzi ya Mungu katika maisha ya kila siku!
Ubarikiwe sana katika Mwaka huu Mpya, Wewe uliyeungana kabisa na Ukombozi wa Mwanao!
Usalimiwe sana, Wewe uliyepokea salamu ya Malaika wa Bwana kwa unyenyekevu mkubwa na uchaji wa Mungu!
Mama wa Kanisa! Mama wa Parokia yetu ya Kiabakari! Utumulikie njia sisi, Taifa la Mungu Parokiani Kiabakari, tukisafiri katika njia za imani, matumaini na upendo! Utusaidie kuishi katika kweli za Kristo; utusaidie kuishi maisha ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wokovu wa watu wote katika dunia nzima na hasa katika Parokia yetu!
3. Tunapokukabidhi, Mama, ulimwengu mzima, watu wote na mataifa yote, kwa namna ya pekee tunajikabidhi kwako sisi tunaoishi chini ya Ulinzi na Malezi yako bora katika Parokia yetu. Tunajifunga ndani ya Moyo wako Safi!
Ewe Moyo Safi wa Maria! Utusaidie kujishinda na kushinda vitisho vya Yule Mwovu; vitisho vinavyotufanya tuanguke katika maovu ya kila aina na mara nyingi kubaki katika maanguko yetu hayo!
Katika njaa na vita,         utuopoe, ee Mama!
Katika umasikini uliokithiri, utuopoe, ee Mama!
Katika uovu wote, utuopoe, ee Mama!
Katika dhambi zote, hasa dhambi za kuua watoto ambao hawajazaliwa, utuopoe, ee Mama!
Katika hasira, chuki na maonevu yoyote, utuopoe, ee Mama!
Katika dhuluma na unyanyasaji wowote, utuopoe, ee Mama!
Katika dharau na dhihaka kwa Amri za Mungu, utuopoe, ee Mama!
Katika kufuru za Sakramenti za Mwanao, hasa Kitubio na Ekaristi Takatifu,        utuopoe, ee Mama!
Katika kuua dhamiri za watu, hasa za watoto na vijana kwa kuwafundisha maisha yasiyokuwa na maadili mema au kuwakwaza kwa mifano mibaya ya maisha yetu, utuopoe, ee Mama!
Katika kifo kibaya bila kupata huduma ya Padre, utuopoe, ee Mama!
Katika dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, utuopoe, ee Mama!
UTUOPOE, EE MAMA!
Utupokee, ee Mama wa Kristo! Ukipokee kilio hiki cha waumini wote wa Parokia yetu kilichojaa mateso ya kila aina! Utusaidie kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kuishinda dhambi: dhambi ya kila mmoja wetu na dhambi za ulimwengu!
Kwa mara nyingine tena idhihirishwe wazi nguvu isiyopimika ya Ukombozi wa Mwanao: nguvu ya Upendo wenye Huruma! Upendo huo uzuie uovu! Ugeuze dhamiri zetu! Tunaomba katika Moyo wako Safi ionekane tena Nuru ya Matumaini kwa wanaparokia wote! AMINA!
Tendo moja la Rozari: Tendo la Tano la Utukufu – Maria anawekwa Malkia wa Mbingu na Dunia! Maria anawekwa Malkia wa Parokia yetu ya Kiabakari!


No comments:

Post a Comment