Tuesday, March 19, 2013

Divine Mercy Solemnity Program Guide

I have just finished and published the official program guide for the upcoming Divine Mercy Solemnity celebrations, anticipated widely by so many pilgrims in and outside of Diocese of Musoma, in and outside of Tanzania. I have high hopes for this year's Divine Mercy Sunday annual pilgrimage. We will prepare as best as we can here in Kiabakari. The rest we leave up to the Merciful Lord. Here is the program guide for Swahili speakers. For non-swahili speakers I suggest to use Google Translator provided in the right hand sidebar. Welcome to Kiabakari. Join us for the wonderful celebration of God's Mercy!
SHEREHE YA HURUMA YA MUNGU 
Huruma ya Mungu nitaiimba milele !
KITUO CHA KIJIMBO CHA HIJA YA HURUMA YA MUNGU 
PAROKIA YA KIABAKARI, JIMBO LA MUSOMA, TANZANIA

Ijumaa-Dominika, 5-7 Aprili 2013


OMBI: Tunaomba Mahujaji wote wafike Kiabakari wakiwa na Biblia Takatifu, rozari, daftari, kalamu na mche wa mti  (kila kikundi cha Mahujaji, hata Mahujaji binafsi) kama ukumbusho wa hija ya mwaka huu wa 2013.IJUMAA – 5 APRILI 2013


MUDA
TUKIO
4.00-4.45
Sala za asubuhi na Rozari Takatifu
4.45-5.00
Tafakari binafsi
5.00-5.45
Kipindi I
5.45-6.00
Tafakari binafsi
6.00-6.15
Malkia wa Mbingu na Sala ya Mchana
6.15-6.30
Tafakari binafsi
6.30-7.30
Njia ya Msalaba
7.30-8.15
Kipindi II
8.15-9.00
Maandalizi binafsi ya Sakramenti ya Upatanisho
9.00-10.00
Ibada ya Sakramenti ya Upatanisho
10.00-11.00
Saa ya Huruma ya Mungu - Saa Takatifu
(pamoja na Novena ya Huruma ya Mungu – siku ya nane)
11.00-12.00
Misa Takatifu JUMAMOSI – 6 APRILI 2013 
(kuanzia asubuhi hadi saa 2.00 usiku)

Sherehe ya Kuzaliwa Mwenye Heri Petro George Frassati, 
Somo wa Hekalu la Huruma ya Mungu, wa Parokia ya Kiabakari 
na wa Kituo cha Afya Parokiani Kiabakari


MUDA
TUKIO
12.45-1.30
Sala za asubuhi na Rozari Takatifu
1.30-2.30
Misa Takatifu kwa heshima ya Bikira Maria, 
Mama wa Huruma
2.30-6.00
Tafakari binafsi, sala na mapumziko
6.00-6.05
Malkia wa Mbingu na Rozari Takatifu
6.05-9.00
Tafakari binafsi, sala na mapumziko
9.00-10.00
Saa ya Huruma ya Mungu - Saa Takatifu
(pamoja na Novena ya Huruma ya Mungu – siku ya tisa)
10.00-11.00
Tafakari na sala binafsi
11.00-12.00
Misa Takatifu ya kuwakaribisha na kuwabariki Mahujaji
12.00-2.00
Tafakari binafsi, sala na mapumziko


MKESHA WA SHEREHE YA HURUMA YA MUNGU
6-7/04/20103

(kuanzia saa 2.00 usiku Jumamosi hadi saa 12.00 alfajiri siku ya Dominika)

Angalisho: Huduma ya Sakramenti ya Upatanisho kwa mahujaji watakaowasili Kiabakari siku ya Jumamosi jioni itatolewa kuanzia saa 3.00 usiku hadi watakapoisha. Waamini wa Parokia ya Kiabakari na mahujaji watakaoshiriki mafungo ya Ijumaa ya tarehe 5.04.2013 wanaombwa waungame siku ya Ijumaa wakati wa mafungo ama Jumamosi kabla ya Misa ya asubuhi – ili kuwapa nafasi mahujaji wengine kuungama wakati wa mkesha na hivyo kuepuka msongamano mkubwa wa waungamaji.


MUDA
TUKIO
2.00-2.10
Maandamano ya Kusimika Patakatifuni Masalia ya Msalaba Mtakatifu, Mwenye Heri Yoahne Paulo II na Mtakatifu Faustina Kowalska
2.10-2.55
Ufunguzi wa Mkesha na Kipindi I
2.55-3.00
Maandalizi ya Maandamano ya Mwanga wa Matumaini 
na ya Rozari Takatifu
3.00-5.00
Maandamano ya Mwanga wa Matumaini na ya Rozari Takatifu 
Badala ya kulaani giza, tuwashe mishumaa ya matumaini!’
5.00-5.45
Kipindi II
5.45-6.00
Maandalizi ya Misa Takatifu
6.00-7.30
Misa Takatifu kwa heshima ya 
Mt. Sista Faustina Kowalska wa Ekaristi Takatifu 
7.30-7.45
Mapumziko, tafakari binafsi, sala
8.00-9.00
Njia ya Msalaba
9.00-9.15
Mapumziko, tafakari binafsi, sala
9.15-9.30
Ibada ya Kubariki Maji na Kufungua Kisima cha Ubatizo 
9.30-11.00
Ibada ya Kurudia Ahadi za Ubatizo na Kumuenzi Mtakatifu Somo
11.00-1.00 asubuhi
Mkesha wa vikundi vya mahujajiDOMINIKA YA SHEREHE YA HURUMA YA MUNGU 
7/04/2013MUDA
TUKIO
1.00-2.30 asubuhi
Mapumziko, tafakari binafsi, sala
2.30-3.30
Ibada ya Kubariki Maji na Kufungua Kisima cha Ubatizo, 
Sala za asubuhi na Rozari Takatifu
3.30-4.00
Maandalizi ya Misa Kuu ya Sherehe
4.00-6.30
Misa Kuu ya Sherehe ya Huruma ya Mungu 
pamoja na Ibada ya Kusimika rasmi tawi la kwanza la  Mitume wa Huruma ya Mungu (Parokia ya Tarime) na Ibada ya Huruma ya Mungu
6.30-7.00
Kupanda miti ya ukumbusho wa Sherehe ya Huruma ya Mungu 
katika Mlima wa Huruma ya Mungu
7.00-----
Mandalizi ya safari ya
kurudi nyumbani na kuondoka


ANGALISHO MUHIMU: 

Mahujaji wote wazingatie kwamba hija ni zoezi la kiroho linaloambatana na matendo ya kujinyima, kujikatalia, kutubu na kuzama kwa sala katika kilindi cha Bahari ya Huruma ya Mungu. Ni safari ya wongofu wa mwana mpotevu anayerudi kwa Baba Aliye Mwingi wa Huruma. Tunaomba mahujaji wote watilie maanani na kuzingatia kwa dhati ukweli huo kusudi sote kwa pamoja tuweze kuadhimisha Sherehe ya Huruma ya Mungu katika mazingira tulivu ya roho ya sala na uchaji wa Mungu wa hali ya juu na hivyo tuwe tayari kujichotea Huruma ya Mungu katika Bahari ya Huruma yake na kupokea neema za pekee zilizoandaliwa na Mwenyezi Mungu Aliye Mwingi wa Huruma kwa wote watakaozingatia mashauri haya na kukaribia Kiti cha Huruma yake katika Mlima wa Huruma yake Kiabakari kwa moyo wa toba, unyenyekevu, imani hai, matumaini yasiyotikisika na upendo wa dhati. 

Kituo cha Hija, kwa kuzingatia idadi kubwa ya mahujaji washiriki na hitaji la kusogeza huduma hizo muhimu karibu zaidi nao, kimetoa kibali kwa wenyeji kuuza maji ya kunywa, soda, vyakula n.k. karibu na Mlima wa Huruma ya Mungu – kwa gharama za kawaida.  

Aidha, katika duka la vitabu la Kituo cha Hija vitapatikana vitabu vya Huruma ya Mungu na vinginevyo, picha za Yesu, Mfalme wa Huruma, vijitabu vya mwongozo wa Sakramenti ya Upatanisho, Shahada za Mahujaji, rozari, medali, skapulari, vitenge vya Mwaka wa Imani,  polo shirts (mabeloni) za Kituo cha Hija n.k. 

Viongozi wa kila kikundi cha Mahujaji wanaombwa kufika ofisini mara baada ya kuwasili Kiabakari kwa ajili ya kuviandikisha vikundi vyao katika Rejesta ya Kituo cha Hija na kupata utaratibu mzima kutoka kwa Wahudumu wa Kituo cha Hija. Mahujaji binafsi wanaombwa pia kufika ofisini kujiandikisha na kuelekezwa na Wahudumu hao.  


Karibuni sana!
Huruma ya Mungu nitaiimba milele!

RATIBA HII IMEANDALIWA NA KITUO CHA KIJIMBO CHA HURUMA YA MUNGU, 
PAROKIA YA KIABAKARI, JIMBO LA MUSOMA, TANZANIA. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.

No comments:

Post a Comment